.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumapili, 30 Novemba 2014

TANZANIA 50 PLUS CAMPAIGN WATEMBELEA WAGOJWA WA SARATANI WALIOLAZWA HOSPITAL YA OCEAN ROAD

Mgeni rasma ambaye ni Dr kutoka Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Amana DR. Natalius Kapilima akikata utepe kuashilia kugawa zawadi mbalimbali kwa wagojwa wa saratani waliolazwa katika hospital ya Ocean Road wengine kushoto ni Mkurugenzi wa TTCF. Lutgard Kagaruki na wa tatu kulia ni Mratibu wa kampeni ya manusura wa saratani ya Tezi Dume na Mwanzilishi wa Tanzania 50 Plus Campaign Dr Emanuel Kandusi.
Dk. kutoka Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Amana Dr. Natalius Kapilima kulia akimkabizi zawadi mgojwa wa saratani Idd Muhode ambaye amelazwa katika hospitali ya Ocean Road.
Baadhi ya wadau mbalimbali wa kujitolea kutoka Tanzania 50 plus campaign wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kutoa misaada mbalimbali kwa wagojwa wa saratani katika hospital ya Ocean Road.
Dr kutoka Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Amana Dr. Natalius Kapilima akipokea zawadi za wagojwa zilizoenda kugawiwa katika hospitali ta Ocean Road kutoka kwa Mratibu wa kampeni ya manusura wa saratani ya Tezi Dume na Mwanzilishi wa Tanzania 50 Plus Campagn Dr Emanuel Kandusi mwingine ni Mkurugenzi wa TTCF. Lutgard Kagaruki walipokwenda kutoa misaada mbalimbali kwa wagojwa.
Vifurushi vya zawadi vikiwa tayari kwa kugawiwa kwa wagojwa wa saratani katika hospitali ya Ocean Road.

MKE WA KIPINGU AMWAGA MISAADA SHULE ZA MONTESORY, ULONGONI B AJITOLEA KUFUNZA MICHEZO BURE


Mkurugenzi wa Zugo Gold Mining na Mwakilishi wa Wanawake, Maendeleo ya Vijana na Ajira kwa Wachezaji wa Shirikisho na Ngumi za Ridhaa Tanzania (*BFT), Zuwena Idd Kipingu akizungumza na wazazi kwenye hafla ya Mahafali ya 35 Shule ya Montesoty Nursery& Primary iliyofanyika leo.

Mkurugenzi wa Zugo Gold Mining na Mwakilishi wa Wanawake, Maendeleo ya Vijana na Ajira kwa Wachezaji wa Shirikisho na Ngumi za Ridhaa Tanzania (BFT), Zuwena Idd Kipingu akizungumza na wazazi kwenye hafla ya Mahafali ya 35 Shule ya Montesoty Nursery& Primary iliyofanyika leo.

Baadhi ya wazazi waliohudhuria Mahafali ya 35 ya Shule ya Montesory wakifuatilia maonyesho ya watoto wao.
Baadhi ya wahitimu wa shule ya Montesory wakionyesha maonyesho ya kitaaluma.

                        Ikafuata burudani na kurudi 'magoma' hawa majamaa ni noma.

Babu na wajukuu zake wakisimuliana hadithi kwa vitendo, Kuku na Bata wakimsikiliza Tembo.

KOCHA WA MANCHESTER UNITED ASIFIA KIWANGO KILICHOONYESHWA JANA NA TIMU YAKE


Kocha wa Manchester United, Louis van Gaal amesema anahisi ushindi wa jana wa mabao 3-0 dhidi ya Hull City umetokana na kiwango kizuri cha uchezaji kilichoonyeshwa kwa mara ya kwanza na wachezaji wake katika msimu huu.

Katika mchezo huo Manchester United ilimiliki mpira kwa asilimia 76, wakati wakipata ushindi wao wa tatu mfululizo katika Ligi Kuu ya Uingereza, na kukaa katika nafasi ya nne ya msimamo wa ligi hiyo.

Pia kocha Louis van Gaal ameonyesha kufurahishwa na kitendo cha mchezaji Van Persie kufunga goli katika mchezo huo, hata hivyo Manchester United imejikuta ikipata pigo baada ya Angel Di Maria kuumia.
Nayo Chelsea imejikuta ikibanwa ugenini sare ya 0-0 na Sunderland huku mshambuliaji wake nyota Diego Costa akinusurika kulambwa kadi nyekudu kutokana na kucheza faulu kadhaa za kupiga kiwiko wenzake pamoja na kumpiga teke la shingo mmoja wa wachezaji wa Sunderland.

TAARIFA YA BENKI YA BIASHARA YA MKOMBOZI JUU YA SAKATA LA ESCROW

Taarifa ya benki ya biashara ya Mkombozi juu ya sakata la Escrow

Utangulizi

Taarifa hii inatolewa kwa umma kutokana na ripoti mbalimbali zilizotolewa na baadhi ya vyombo vya habari mitandao ya kijamii na taarifa iliyotolewa kwenye mjadala katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

1. Ufunguzi wa akaunti ya VIP engineering and Marketing (VIP)

Kampuni ya VIP engineering and Marketing ni kampuni ambayo imesajiliwa kwa mujibu wa sheria za Tanzania. Kampuni hii ilifungua akaunti katika benki ya biashara ya Mkombozi na hivyo kuwa moja kati ya wateja wa benki. Benki ilijiridhisha na ilizingatia taratibu zote za ufunguzi wa akaunti husika kwa kuzingatia sheria za nchi na kanuni zinazozitaka benki kupata nyaraka muhimu kutoka kwa mteja wakati wa ufunguzi wa akaunti hiyo.

Nyaraka hizo ni pamoja na kuwepo kwa cheti cha usajili wa kampuni, kanuni za kampuni, idhinisho la kampuni kumruhusu moja kati ya wanahisa wake kuendesha akaunti pamoja na picha na hati ya kusafiria ya mhusika wa kuendesha akaunti hiyo.

2.0 Mauzo ya hisa za VIP

Kampuni ya VIP ilileta mkataba kwenye benki ya Mkombozi wa mauziano ya hisa za asilimia 30 baina ya VIP na kampuni ya Pan Africa Power Solutions (PAP) ambazo inamiliki katika kampuni ya IPTL. Mkataba huo ulisainiwa tarehe 19 Ogasti, 2013. Bei ya asilimia 30 ya hisa hizo ilikuwa ni dola za Marekani milioni 75. Katika kifungu namba 2.4 cha mkataba wao kinaelekeza fedha za mauzo ya hisa zilipwe kwenye akaunti ya VIP iliyopo benki ya Mkombozi. Mkataba huo wa mauziano ya hisa baina ya kampuni hizi mbili ulitambuliwa na hukumu ya Mahakama Kuu ya Tanzania iliyotolewa na Jaji J.H.K Utamwa tarehe 5 Septemba, 2013.

3. Mchakato wa kulipa kodi ya serikali

Benki ilitambua kwamba katika mauziano hayo ya hisa ni lazima kodi ya Serikali ilipwe na hivyo iliizishauri pande zote mbili kupeleka mkataba husika katika ofisi za Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) ili kufanyiwa makadirio ya kodi husika. Tarehe 20 Januari, 2014 TRA iliiandikia barua kampuni ya VIP na nakala ya barua hiyo kuletwa kwenye benki ya Mkombozi. Katika barua hiyo TRA iliitaarifu kampuni ya VIP kuwa makadirio ya kodi yatokanayo na mauzo ya hisa ni shilingi 38,186,584,322.00 ikiwa ni kodi ya mauzo ya hisa ya asilimia 30 za mauzo ya hisa kutoka VIP kwenda kwa PAP.(Capital gains and stamp duty).

TRA pia iliiagiza benki ya Mkombozi kuhakikisha kuwa inalipa kodi hiyo kwa niaba ya VIP mara tu fedha zitakapoingia kwenye akaunti yake.

Malipo ya kodi ya shilingi 38,186,584,322.00 yalilipwa TRA kwenye akaunti 11120100 iliyopo katika Benki Kuu ya Tanzania na TRA ilikiri kupokea kodi hiyo kwa barua yake yenye kumbukumbu namba 3-4/100/100/223/4 ya tarehe 24 Januari, 2014.

4. Ufafanuzi wa mambo mbalimbali

4.1 Benki ya mkombozi kuhusika katika kusafisha fedha chafu

Fedha zote zilizoingizwa kwenye akaunti ya VIP iliyopo kwenye benki ya Mkombozi zilitokana na mauziano ya hisa kati ya VIP na PAP kwa mkataba uliotambuliwa na Mahakama Kuu ya Tanzania. Chanzo cha malipo hayo ni kuhamisha fedha kutoka kwenye akaunti ya PAP iliyopo katika benki ya Stanbic na kuingizwa kwenye akaunti ya VIP iliyopo katika benki ya Mkombozi.

Fedha hizo zilihamishwa katika mafungu mawili. Fungu la kwanza ilikuwa ni shilingi 73,573,500,000.00 zilihamishwa kwa njia ya TISS kwa kumbukumbu namba 000000050720 ya tarehe 23 Januari, 2014 na fungu la pili ni dola za Kimarekani 22,000,000.00 zilihamishwa kwa TISS kwa kumbukumbu namba000000050812 ya tarehe 23 Januari, 2014. Malipo mengine ya asilimia kumi ya mauzo ya hisa yalilipwa kwenye akaunti ya Mkombozi iliyopo Benki Kuu ya Tanzania. Kutokana na mchakato huo benki ya Mkombozi ilijiridhisha kuwa fedha hizo ni malipo halali na siyo fedha chafu.

POLISI KENYA WAMSHIKILIA MUINGEREZA KWA KUHUSIKA NA KIFO CHA MPENZI WAKE

Polisi nchini Kenya inamshikilia mwanaume mmoja raia wa Uingereza kwa kuhusika na kifo cha mpenzi wake mwenye maradhi ya kisukari, baada ya kuziflashi chooni dawa zake katika nyumba wanaoishi iliyopo Gachie, Jijini Nairobi.

Kwa mujibu wa polisi Muingereza huyo Carl Cary Singleton mwenye umri wa miaka 41, aliteketeza dawa za mchumba wake huyo raia wa Kenya, na kumzuia ndani ya nyumba hiyo kwa siku mbili baada ya kumpiga.

Vyombo vya habari vya Uingereza vimesema Singleton walijuana kwa mara ya kwanza na mpenzi wake huyo Peris Ashley Agumbi Mumtah aliyekuwa anasoma Chuo Kikuu cha Nairobi kampasi ya Lower Kabete kwa njia ya mawasiliano ya Facebook.

BONDIA TYSON FURY AMDUNDA DERECK CHISORA NA KUTWAA MIKANDA MIWILI

Bondia Tyson Fury ameshinda mataji mawili ya mkanda wa uzito wa juu wa Uingereza na Ulaya, katika raundi ya 10 kwenye pambano lake na bondia aliyesalimu amri Dereck Chisora kwenye ukumbi wa ExCel arena, Jijini London.

Bondia huyo wa Manchester, Fury, ambaye alimzidi pinti Chisora mwaka 2011, alibadili staili ya kupigana katika raundi ya pili na kumudu kutawala kila dakika ya mchezo huo katika kila raundi.

Bondia Chisora ambaye makazi yake yapo London, katika mchezo huo alionekana kabisa kushindwa kuonyesha makali yake, na pia kushindwa kudhibiti makombora ya mpinzani wake Tyson Fury.

Kwa ushindi huo Fury anajipanga kupigana na bingwa anayeshikilia mikanda ya uzito wa juu ya WBA, IBF na WBO mrusi Wladimir Klitschko. 
                                        Tyson Fury akimpa uppercut bondia Dereck Chisora
                    Bondia Dereck Chisora hoi akipatiwa tiba katika jeraha alilopata
   Refa wa pambano hilo akitoa ishara ya kumaliza pambano katika raundi ya kumi

AFISA WA REBUPLICAN AOMBA RADHI BAADA YA KUWASHUTUMU MABINTI WA RAIS OBAMA

Mabinti wa Rais Barack Obama, Sasha na Malia wametuhumiwa kuonyesha kutokuwa na heshima na hawana viwango na afisa mmoja wa chama cha Republican baada ya kuonekana katika hafla ya sherehe za Thanksgiving wakiwa wamevalia vimini.

Afisa huyo Elizabeth Lauten, ambaye ni mkurugenzi wa mawasiliano wa mjumbe wa Baraza la Congress Stephen Fincher, aliandika hayo kupitia ukurasa wake wa Facebook, na kisha kufuta, baada ya kushambuliwa mno kwa kutoa maneono yenye kuumiza, ambapo pia ameomba msamaha.

Lauten aliwatuhumu pia mabinti hao wa rais Obama, walionekana wakiwa wameboreka wakati wakiwa wamesimama pamoja na baba yao, katika kitendo cha utumaduni wa Ikulu kuwaachia huru batamzinga wawili ili kuwaepusha kutumika kama mlo wa jioni wakati wa sherehe za Thanksgiving.

DAVID BECKHAM APATA AJALI NA MWANAE AKITOKEA KWENYE DIMBA LA ARSENAL

                                              Brooklyn akiwa na baba yake David Beckham

Mwanasoka veterani wa Uingereza David Beckham amepata ajali ya gari leo asubuhi wakati akienda kumchukua mtoto wake Brooklyn katika uwanja wa mazoezi ya mpira vya klabu ya timu ya Arsenal.

Beckham, 39, alikuwa katika uwanja huo wa mazoezi wa London Colney, Hertfordshire, akimuangalia mtoto waki huyo mkubwa wa kiume Brooklyn, 15, akichezea timu hiyo ya wachezaji chini ya miaka 16 dhidi ya Brighton.

Hata hivyo katika ajali hiyo kapteni huyo wa zamani wa timu ya taifa ya Uingereza na mwanae Brooklyn hawakupata majeraha yoyote, licha ya gari lao kuharibika na kulazimika kutumia gari lingine.
David Beckham akiwa na watoto wake wa liume Brooklyn (kushoto), Cruz (katikati) na Romeo (kulia).

POLISI WA MAREKANI ALIYEMUUA KIJANA MWEUSI HUKO MISSOURI AJIUZULU

Afisa polisi wa Marekani Darren Wilson aliyempia risasi na kumuua kijana mweusi asiye na silaha Michael Brown huko Missouri katika Mji wa Ferguson amejiuzulu wadhifa wake, wakili wake Neil Bruntrager amesema.

Wakili Bruntrager ameviambia vyombo vya habari nchini Marekani uamuzi huo wa mteja wake kujiuzulu wadhifa polisi umeanza mara moja.

Polisi huyo Wilson amenukuliwa akisema amechukua uamuzi huo kutokana na tishio la kuendelea kwa ghasi iwapo ataendelea kuwa ndani ya jeshi la polisi.

Mji wa Ferguson pamoja na miji mingine ya Marekani imejikuta katika ghasi na maandamano kufuati uamuzi wa mahakama kuamua polisi huyo hapaswi kufunguliwa mashtaka.

RAIS KIKWETE AWASILI DAR ES SALAAM, APATA MAPOKEZI MAKUBWA

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na mmoja wa abiria wakati ndege aliyopanda ilipotua katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es salaam akitokea Marekani kwenye matibabu leo Novemba 29, 2014
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Katibu wa Rais Bw. Morris Mbena baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es salaam akitokea Marekani kwenye matibabu leo Novemba 29, 2014
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Mama Salma Kikwete wakiwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es salaam akitokea
Marekani kwenye matibabu leo Novemba 29, 2014
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na baadhi ya wafanyakazi katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es salaam baada ya kuwasili akitokea Marekani kwenye matibabu leo
Novemba 29, 2014
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwapungia mkono wafanyakazi katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es salaam baada ya kuwasili akitokea Marekani kwenye matibabu leo Novemba 29, 2014
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Mkuu wa Majeshi Jenerali davis Mwamunyange baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es salaam akitokea Marekani kwenye matibabu leo Novemba 29, 2014
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Mkuu wa Jeshi la Polisi IGP Ernest Mangu baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es salaam akitokea Marekani kwenye matibabu leo Novemba 29, 2014
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Kamishna Jenerali wa Magereza John Minja baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es salaam akitokea Marekani kwenye matibabu leo Novemba 29, 2014
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Usalama Bw. Rashid Othman baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es salaam akitokea Marekani kwenye matibabu leo Novemba 29, 2014
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Mama Maria Nyerere baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es salaam akitokea Marekani kwenye matibabu leo Novemba 29, 2014

ZAHRA MUHIDIN MICHUZI ALAMBA NONDOZI YAKE UDOM

Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dodoma,Rais Mstaafu wa awamu ya tatu,Mh. Benjamin W. Mkapa akiongoza mahafali ya tano ya Chuo Kikuu hicho yaliyofanyika leo katika eneo la Chimwaga,ndani ya Chuo Kikuu cha Dodoma leo.
Sehemu ya Wahitimu wa Chuo Kikuu cha Dodoma wakiwa kwenye mahafali hayo mara baada ya kutunukiwa Shahada zao mbali mbali leo.wa pili kushoto ni Mtoto wa Ankal bi. Zahra Muhidin Michuzi.

AJALI YA HELIKOPTA YA MALI ASILI ILIYOTOKEA JANA

                                                     Sehemu ya mabaki ya Helikopta baada ya kuanguka
Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Suleiman Kova
akifafanua jambo mbele ya Vyombo vya habari katika eneo la ajali,kufuatia kutokea kwa ajali hiyo iliyopelekea vifo vya watu wanne
Mkuu wa Mkoa wa Dar Es Salaa,Mh.Sadick Meck Sadick akizungumza mbele ya Vyombo vya habari katika eneo la ajali,kufuatia kutokea kwa ajali hiyo
iliyopelekea vifo vya watu wanne
Baadhi ya Wataalamu wakifanya uchunguzi wa chanzo cha ajali hiyo ya Helikopta.
Baadhi ya Watu wakishuhudia mabaki ya helikopta hiyo iliyopata ajali maeneo ya Kipunguni B Moshi Bar,Ilala jijini Dar es
Salaam. Helikopta hiyo inamilikiwa na Wizara ya Mali Asili na Utalii.

Jumamosi, 29 Novemba 2014

HELKOPTA YA TANAPA YAANGUKA, WATU WOTE WANNE WALIOKUWA NDANI YAKE WAMEFARIKI DUNIA

Picha na maktaba. 

Helkopta inayosemekana inamilikiwa na TANAPA imeanguka na kuteketea kwa moto katika eneo la Kipunguni jijini Dar es Salaam leo asubuhi. 

Kwa mujibu wa mashuhuda, wamesema waliona helkopta hiyo ikipoteza uelekeo na badaye kuanguka chini hali iliyosababisha kishindo kikubwa baada ya kulipuka moto. 

Inasemekana ndani ya helkopta hiyo kulikuwa na watu wanne na wote wamepoteza maisha. Tutawapa taarifa zaidi.

BUNGE LAHAIRISHWA TENA HADI SAA KUMI JIONI

Bunge limehairishwa kwa mara ya pili leo, sasa litakaa saa kumi jioni ili kutoa muda kwa kamati kuendelea kusaka maridhiano, ili Bunge litakapokaa jioni muafaka uweze kufikiwa bila kuwepo na mivutano. 

Mh Spika Anne Makinda amefikia uamuzi huo baada ya kuombwa bunge kuahirishwa kwa saa moja na Waziri wa Nchi, Mh William Lukuvi ili wabunge wa CCM waweze kukutana na kuafikiana ili bunge likapokaa tena waweze kuwa wamoja kwa mustakabali wa nchi yetu. 

Hata hivyo Mh Zitto Kabwe yeye aliomba masaa mawili, Mh Mbatia akaomba wapewe muda zaidi, na katika kuhitimisha, Mh Spika akasema bunge litakutana saa kumi jioni.

WAGENI KUTOKA NANJING CHINA WATEMBELEA OFISI ZA WIZARA YA HABARI, VIJANA, UTAMADUNI NA MICHEZO

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Haabari, Vijana Utamaduni na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel kushoto akizungumza na watu kutoka Jamhuri ya watu wa china (hawapo pichani) walipofika katika ofisi za Wizara kuonana na uongozi wa Wizara kabla ya Maonyesho ya Miaka 50 ya ushirikiano kati ya Tanzania na China yaliyofanyika jioni yake. Kulia ni Mkurugenzi msaidizi Sanaa Bibi Leah Kihimbi.
Mkuu wa masuala ya Utamaduni, Utangazaji, Habari na Uchapishaji kutoka Nanjing China Bw. Yan Yiping kushoto akifafanua jambo walipofika katika ofisi za Wizara kuonana na uongozi wa Wizara kabla ya Maonyesho ya Miaka 50 ya ushirikiano kati ya Tanzania na China yaliyofanyika jioni yake. Kulia ni Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Haabari, Vijana Utamaduni na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel.
Baadhi ya wageni kutoka Nanjing China wakifuatilia mazungumzo yaliyokua yakiendelea walipofika katika ofisi za Wizara kuonana na uongozi wa Wizara kabla ya Maonyesho ya Miaka 50 ya ushirikiano kati ya Tanzania na China yaliyofanyika jioni yake. Kushoto ni Mkurugenzi msaidizi Mila Bibi Lily Beleko.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Haabari, Vijana Utamaduni na Michezo Prof.Elisante Ole Gabriel kulia akipokea zawadi kwa niaba ya Wizara kutoka kwa Mkuu wa masuala ya Utamaduni, Utangazaji, Habari na Uchapishaji kutoka Nanjing China Bw. Yan Yiping walipofika katika ofisi za Wizara kuonana na uongozi wa Wizara kabla ya Maonyesho ya Miaka 50 ya ushirikiano kati ya Tanzania na China yaliyofanyika jioni.

                                                                       Picha na Genofeva Matemu - Maelezo

BOKO HARAMU WAHUSISHWA ULIPUAJI WA MSIKITI MJINI KANO AMBAPO WATU 120 INASADIKIWA KUFARIKI DUNIA

Inasadikiwa kuwa zaidi ya waumini 120 wamefariki dunia na wengine zaidi ya 270 wamejeruhiwa baada ya kutokea milipuko ya mabomu wakati wakiwa katika ibada ya ijumaa katika msikiti mkuu wa Grand uliopo mjini Kano nchini Nigeria jana mchana.
Mabamu matatu yanasemekana kulipuliwa katika msikiti huo, na bomu la kwanza lililipuka wakati mshambuliaji alipokuwa anataka kuingia na gari ndani ya maegesho ya magari ya msikiti huo. 

Wapiganaji wa kundi la Boko Haramu wanahusishwa na tukio hilo la kuhuzinisha.
Kundi la Boko Haramu limekuwa likifanya vitendo vya utekaji na mauaji ya mara kwa mara katika maeneo mbalimbali nchini Nigeria.
Moshi mkubwa ukionekana kutanda katika eneo la msikiti huo huku wananchi wakishuhudia.